Jeshi la Polisi Lamtaka Benard Morrison Kufika Kituoni Mbweni

Jeshi la Polisi Lamtaka Benard Morrison Kufika Kituoni Mbweni


Jeshi la Polisi kupitia taarifa yake limetoa ufafanuzi baada ya aliyekuwa mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Simba, Bernard Morrison kulituhumu jeshi hilo kituo cha Mbweni kuwa linachukua rushwa, likimtaka staa huyo kufikia kituo hapo.

Morrison raia wa Ghana, alisambaza taarifa katika mitandao ya kijamii akikituhumu kituo cha Polisi Mbweni kuwa polisi wake wanachukua rushwa na wanafanya kazi kwa maslahi yao binafsi.

"Kuna watu wanafanya kazi kwenye kituo cha Mbweni hawasaidii watu wenye shida na wana maslahi yao binafsi, wanajichukulia sheria mkononi na kufanya wanavyotaka, ikiwa mimi ninayejua vizuri ninaweza kutapeliwa na kutoheshimiwa unafikiri wananchi wa kawaida wanaweza kufanyaje," ilisema taarifa ya Morrison.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi kupitia taarifa iliyotolewa leo desemba 19.2024 kupitia na Msemaji wake David Misime imesema kuwa Morrison anatakiwa kusema ukweli.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad