Jeshi la Polisi Limetoa Ufafanuzi Rasmi Juu ya Kashfa ya Benard Morrison


Jeshi la Polisi limetoa ufafanuzi rasmi juu ya taarifa inayosambaa mitandaoni ikimhusisha mchezaji Bernard Morrison na Kituo cha Polisi Mbweni.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, Morrison aliwasilisha malalamiko ya wizi wa kuaminiwa mnamo Machi 2024.



Morrison alieleza kuwa akiwa Ghana, alimtuma Abdul Rakeeb Mgaya kiasi cha shilingi milioni moja na laki tano (1,500,000) ili fedha hizo zimfikie mdogo wake, anayejulikana kama Boat, aliyeko Tanzania.

Lengo lilikuwa kumpa msaada Boat ili kutafuta klabu ya soka itakayomsajili.

Hata hivyo, Mgaya anadaiwa kushindwa kutekeleza jukumu hilo, hali iliyosababisha Morrison kufungua malalamiko rasmi katika Kituo cha Polisi Mbweni.

Jeshi la Polisi limeweka wazi kuwa uchunguzi juu ya suala hilo ulianza mara moja baada ya malalamiko kupokelewa.

Aidha, limewataka wananchi kuacha kusambaza taarifa zisizo sahihi au zenye kupotosha, kwani zinalenga kuchafua taswira ya vyombo vya dola na wahusika.

Kwa mara nyingine, Jeshi la Polisi limehimiza matumizi ya mitandao ya kijamii kwa uwajibikaji na kuepuka kueneza uvumi usio na msingi.


Licha ya ukweli wa suala hilo kuwekwa bayana, Bernard Morrison hajazungumza lolote kuhusu sakata hilo mitandaoni, akibaki kimya huku wafuasi wake wakitoa maoni mseto.

Jeshi la Polisi limeahidi kuendelea kutoa taarifa rasmi pale panapohitajika. Wamesisitiza kuwa suala hilo linasimamiwa kwa umakini na kwa mujibu wa sheria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad