Jinsi Kocha Fadlu Davids Anavyowachanganya Wapinzani, Yaani Nabi Mtupu

Jinsi Kocha Fadlu Davids Anavyowachanganya Wapinzani, Yaani Nabi Mtupu


Anachokifanya kocha Fadlu Davids ni kuwachanganya wapinzani, wakati wakijiandaa kumkaba Leonel Ateba yeye anamuanzisha Dese Mukwala, wakati wapinzani wakifikiria jean Charles Ahoua ataanza kama namba 10,yeye anamuweka Awesu Awesu kama inside 10 halafu Jean Charles Ahoua kama half space midfielder.

Hapo bado kwenye kiungo cha chini ,bado mbavu ya kushoto na kulia+CB’s,eneo pekee lenye mtu wa kudumu ni golikipa Mousa Camara.

Hapa ndio nimeanza kumkumbuka kocha Nasredine Nabi, alifanikiwa ndani ya Yanga Sc kwa style kama hii hii anayefanya Fadlu Davids.

Kila mchezaji ana nafasi kwake,hana hiyana kazi inabaki kwa mchezaji ku prove kwake ili aendelee kucheza kwenye kikosi chake.

Kwa mwenendo huu Fadlu Davids ataendelea kunufaika na wachezaji wake kwasababu kila mmoja anaimani akifanya vizuri kiwanja cha mazoezi ataweza kupata nafasi ya kucheza mechi.

Kwenye hili namuona Nabi ndani ya Fadlu Davids

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad