Kwa sasa ukitaja sehemu ambayo wasanii wa Bongo Fleva wanavuna sana pesa huenda ikawa ni Kenya inaongoza kwa wasanii wa Bongo Fleva kulipwa zaidi.
Ukiachana na show nyingi ambazo wasanii wa Bongo Fleva wanafanya Kenya, majuzi tuliona story ya Diamond kulipwa milioni 400 Tamasha la Fursha Fest.
Leo hii Diamond amelipwa dola milioni moja kwenye harusi ya kifahari Mombasa kwenda kutumbuiza ambayo ni sawa na Tsh bilioni 2.3
Ukiachana na Diamond Nandy majuzi alikuwa Mombasa ambapo ameeleza kulipa dola laki 350 ambapo ni zaidi ya Tsh milioni 839 kwa show ya Dakika 10 tu.
Mbali ya kuwa Wasanii wa Bongo Fleva wanalipwa zaidi Kenya pia tukubali kuwa Wakenya wanawapenda wasanii wa Bongo Fleva mno.
Ukiacha wasanii wa Bongo Fleva kupendwa Kenya pia Wakenya wanaonekana wana Pesa sana maana wasanii wanalipwa na watu binafsi tu.
Unahisi kwa Tanzania kwenye Harusi msanii wetu mkubwa anaweza kulipwa bei gani??