Kenya Yalipa Milion 500 KSH Ili Kuandaa Tuzo za Grammy

Kenya Yalipa Milion 500 KSH Ili Kuandaa Tuzo za Grammy


Rais William Ruto wa Kenya, ameweka wazi kwamba Kenya imewasilisha rasmi ombi la kuwa mwenyeji wa Grammy Awards na tayari imelipa Ksh. milioni 500 kufanikisha azma hiyo.


Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC), kuadhimisha miaka miwili ya serikali ya Hustler, Rais Ruto alisisitiza dhamira ya serikali yake kuimarisha tasnia ya ubunifu na kuiweka Kenya kama kitovu cha burudani duniani.


Mwezi Aprili, Rais Ruto alitangaza kuwa Kenya ni miongoni mwa nchi nne zilizochaguliwa kushiriki Grammys kupitia ushirikiano na Grammy Global Ventures, hatua inayolenga kuimarisha ushiriki wa Kenya katika tasnia ya ubunifu ya kimataifa.


Kwa upande wake, Dennis Itumbi, Mkuu wa Miradi Maalum ya Rais na Uchumi wa Ubunifu, alithibitisha kwamba ofisi yake imeagiza Wizara na Serikali kuwezesha malipo ya ombi la Kenya kuwa mwenyeji wa Grammy Awards za Afrika.


Itumbi pia alidokeza kuwa mwakilishi wa Grammy Awards aliyekuwepo katika mkutano huo atakutana na Rais Ruto wiki hii kuzungumzia suala hilo.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad