Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati amethibitisha kupokea taarifa kuhusu kifo cha Juliana Obedi (43) ambaye alifariki baada ya kung’atwa na Nyoka na kucheleweshewa matibabu kwa tuhuma za kukosa fedha za matibabu ambapo tukio hili lilitokea katika Kituo cha Afya Magugu ambapo Juliana alicheleweshwa kufanyiwa matibabu ya dharura hali iliyosababisha kifo chake.
Kufuatia tukio hili Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati amewasimamisha kazi watoa huduma watatu wa Kituo cha Afya Magugu kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ambapo uchunguzi unaendelea na hatua kali zitachukuliwa kwa wote watakaobainika kuhusika na kuchelewesha matibabu ya dharura.
Halmashauri ya Babati inasisitiza kuwa makundi maalumu kama akina Mama wajawazito na Watoto chini ya miaka mitano wanatakiwa kupatiwa matibabu bure pia Mkurugenzi ametoa wito kwa Jamii kuhakikisha wanapata huduma za kiafya mapema hasa wakati wa dharura.
Aidha Halmashauri hiyo imetoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Marehemu Juliana kwa msiba huu mzito.