Mbeya City vs Geita Gold.
Kocha wa makipa wa klabu ya Gita Gold, Augustino Malindi amefungiwa michezo 16 (kumi na sita) na kutozwa faini ya Sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kumshika sehemu za siri wamuzi wa akiba wa mchezo tajwa hapo juu.
Baada ya kuonywa kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumtukana mwamuzi msaidizi namba moja (1) wa mchezo huo.
Kocha huyo alitenda kosa lingine akiwa anakwenda vyumbani baada ya kuonywa kwa kadi, kwa kumshika kifuani mratibu wa mchezo huo (GC) ambaye ni mwanamke jambo ambalo ni kinyume na maadili ya ukocha na mpira wa miguu kwa ujumla.
Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 45:2(2.1) ya Ligi ya Championship kuhusu Udhibiti kwa Makocha.
Pia kocha Augustino Malindi amefungiwa michezo mitatu (3) a kutozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kumtukana mwamuzi msaidizi namba moja
(1) wa mchezo huo jambo lililosababisha aonywe kwa kadi nyekundu.
Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 45:2(2.11) ya Ligi ya Championship kuhusu Udhibiti kwa Makocha.