Kocha Ruud Van Nistelrooy Hajawahi Kufungwa EPL

Kocha Ruud Van Nistelrooy Hajawahi Kufungwa EPL


Mpaka sasa watu wengi hawaamini. Je wanachokiona kutoka kwa Ruud Van Nistelrooy ni kismati au uwezo?

Mpaka sasa Ruud Van Nistelrooy hajafungwa mechi yoyote akiwa ndani ya EPL kama kocha.

Mechi zote akiwa na Manchester United kama kocha wa muda hakufungwa, huku timu ikifunga bao kuanzia mbili kila mechi.

Baada ya kutemwa na Man U, Leicester wakamnyakua chap.

Mechi yake ya kwanza alishinda 3-1 vs Westham

Jana alikua ameshapigwa 2-0 mpaka dakika ya 85

Kwa sababu ya ubora wa soka lake la kushambulia kama nyuki, Leicester walifanya come-back ya kibabe ndani ya dakika tano

Dk ya 86 Vardy aliweka kambani

Dk ya 90+1 Reid alifunga bao la 2

Mechi ikaisha 2-2

Mpaka sasa akiwa kocha mkuu ndani ya Uingereza mechi 6, ushindi mara 4, sare 2

Watu wa boli wanauliza; Je Van nistelrooy ana uwezo, au bado anatembelea upepo wa bahati?



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad