Tetesi zinaeleza kuwa Kuna uwezekano Yanga SC wakamtimua kocha wao Sead Ramovic endapo atashindwa kuipeleka timu hiyo hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kocha huyo aliyechukua nafasi ya Miguel Gamondi mwezi aliopita ameanza vibaya kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo ambapo amepoteza michezo miwili dhidi ya Al Hilal Omdurman na MC Alger huku mkononi akiwa bado na mechi nne.
Hii leo timu hiyo itakuwa na kibarua kizito kule jijini Lubumbashi ambapo wataivaa TP Mazembe kwenye mchezo wa tatu wa hatua ya makundi ya michuano hiyo.