Rais wa Kenya, William Ruto amesema Tanzania imeipita Nchi ya Kenya katika huduma za biashara za uagizaji na uingizaji bidhaa katika Nchi za Afrika Mashariki.
Akiongea katika Maadhimisho ya Miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Jijini Arusha, Ruto amesema “Kenya ilikuwa inaongoza kwenye masuala ya mwingiliano wa biashara katika Nchi za EAC kwa upande wa biashara za bidhaa na huduma, leo Tanzania imeipita Kenya na naipongeza Tanzania kwa hatua wanayopiga”
“Rais Museveni amesema hatupo kwenye Jumuiya hii kwasababu tunapendana, ni vizuri kupendana lakini tupo kwenye Jumuiya kwasababu tuna malengo yanayofanana , ili tupige hatua zaidi tunahitaji soko kubwa kwa Wazalishaji wetu na Wafanyabiashara wetu kuuza bidhaa zao na kuwekeza”