Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Taifa Freeman Aikael Mbowe Aliyehudumu katika nafasi hiyo kwa takribani miaka 20 sasa leo Disemba 21, 2024 anatoa msimamo wake kuhusu yeye kuendelea kugombea kiti hicho kwa muhula wa tano au kutokuendelea.
Mwenyekiti Mbowe katikati ya juma alipokea ugeni kutoka kwa wananchama, wakereketwa na baadhi ya viongozi wa kanda mikoa na kipekee Kanda ya Pwani wakimuomba achukue fomu agombee wakisema kuwa chama bado kinamuhitaji Mbowe. Hata hivyo mwenyekiti Mbowe aliomba siku mbili kufikiria suala hilo na kutoa majibu ya ama achukuwe fomu au astaafu uongozi.
Kwa sasa katika chama cha CHADEMA kumueonekana kuwepo na mgawanyiko baada ya Makamu Mwenyekiti wao Tundu Lissu kutangaza nia na baadaye kuchukua fomu ya Uenyekiti Mapema wiki hii.
Tunakuletea matangazo haya ya moja kwa moja kutoka nyumbani kwa mwenyekiti Mbowe Mikocheni jijini Dar es Salaam kuanzia saa tano kama ilivyotangazwa.