Liverpool imeshusha kipigo cha 6-3 ugenini dhidi ya Tottenham Hotspur na kuendelea kujichimbia zaidi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England pointi 39 baada ya mechi 16, pointi nne mbele ya Chelsea waliopo nafasi ya pili.
Mohammed Salah amekuwa mchezaji wa kwanza kwenye historia ya Ligi kuu England kufunga na kutoa pasi saidizi ‘assists’ zaidi ya 10 kabla ya Christmas. Salah amefunga magoli mawili na kutoa ‘assists’ mbili kwenye ushindi huo ikiwa ni jumla ya magoli 15 na ‘assists’ 11 kwenye Ligi mpaka sasa.
FT: Tottenham 3-6 Liverpool
⚽ 41’ Madison
⚽ 72’ Kulusevski
⚽ 83’ Solanke
⚽ 22’ Diaz
⚽ 36’ Mac Allister
⚽ 45+1’ Szoboszlai
⚽ 54’ Salah
⚽ 61’ Salah
⚽ 85’ Diaz