Maandamano ya Kupinga vitendo vya Utekaji yaliyoitishwa na Wanaharakati wa Haki za Binadamu na Ndugu na Jamaa wa Watu walioripotiwa kutoweka katika Mazingira yenye utata, yameanza leo licha ya Jeshi la Polisi kuyaita ni haramu
Hatua hiyo inafuatia kupita Saa 48 za wito wa kuachiwa huru kwa Watu waliotekwa, muda uliotolewa na Wanaharakati kwenda kwa Mamlaka zinazotuhumiwa kuhusika na vitendo hivyo, wakiwemo Maafisa wa Idara za Ulinzi na Usalama wa Serikali
Kwa mujibu wa taarifa iliyosambazwa Mitandao Desemba 29, 2024, Waitishaji wa Maandamano hayo wamesema wataendelea kuandamana bila kukoma hadi pale ndugu zao watakapoachiwa na hawajali itachukua siku ngapi.