Majina ya Waliofariki Katika Ajali ya Gari Tarakea Rombo..




Tarehe 26/12/2024 majira ya saa tisa na dakika arobaini jioni huko kijji cha Kibaoni Tarafa ya Tarakea Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjaro barabara kuu ya Moshi - Tarakea gari lenye namba za usajili T. 620 DZQ Bus Yutong kampuni ya Ngasere ikitokea Dodoma kwenda Tarakea iligongana na gari dogo la abiria lenye namba za usajili T959 CKU Toyota Noah ikitokea Tarakea kwenda Moshi na kusababisha vifo vya watu tisa (9) wote walikuwa kwenye gari namba T959 CKU Toyota Noah.

Waliofariki katika ajali hiyo na waliofahamika ni: -
1. Mamasita Lowasa, (27), mkazi wa Kamwanga.
2. Damarisi Kanini Mwikau, (22), mkazi wa Elast Kenya.
3. Peter Alex Urio, (38).
4. Monica Joyce Mumbua, (64) Mkenya.
5. Eligatanasi Kanje, (30), mkazi wa Tarakea.
6. Hilda Francis Leberatus, (24), mkazi wa Kikelelwa.Mili mingine ya watu watatu haijatambuliwa.

Majeruhiwa mmoja aliyekuwa mtembea kwa miguu majina yake hayajafahamika amepelekwa hospitali ya Huruma Wilaya ya Rombo kwa matibabu.

Uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa gari dogo la abiria Noah kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari.

Miili ya marehemu imehifadhiwa hospitali ya Huruma Wilaya ya Rombo kusubiri uchunguzi na taratibu zingine.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad