Itakuaje Man United vs Everton?
Najaribu kufungua vitabu vyangu vya takwimu, kurasa ya kwanza naiona Everton.
Kwenye mechi 8 zilizopita, Everton kashinda 2, Sare 5, kapoteza 1
Katika mechi zao 8, hakuna hata mechi moja ambayo wameruhusu bao zaidi ya moja. Ni either wafungwe moja, au wamalize mechi 0-0. Na hata ikitokea wameshinda, basi huwa hawashindi kwa zaidi ya tofauti ya mabao mawili.
Kwa kuwa namba hazidanganyi, hii inatupa picha kuwa Everton ni watamu kwenye kuzuia, na wabovu pia kwenye kufunga.
Naifungua kurasa ya pili ya kitabu changu cha takwimu naiona Man United iliyoamua kuanza upya.
Ni Man U ambayo, imecheza mechi 12 za ligi; Imeshinda mechi 4, Kufungwa mechi 4, na kutoa sare mechi 4 mpaka sasa.
Namba hazipo sana upande wa kutuonyesha kuwa Man U ana muendelezo wa ubora. Namba zinatuambia, Man U usimtegemee kwa chochote, anaweza kukuaibisha.
Kuelekea mechi ya kwanza kwa Amorim akiwa nyumbani leo hii vs Everton, wahafidhina wa Mashetani wekundu bado wanataka kujiridhisha zaidi je Amorim ni mtu sahihi kuwafikisha nchi ya ahadi?
Kumbuka Man U vs Ipswich, na Man U vs Bodo, mashabiki bado hawakuelewa kwanini timu yao inaacha nafasi za kushambuliwa sana? Je mfumo wa Amorim na aina ya wachezaji waliopo Man U hauendani?
Lakini bado wengine wanasema, kwa sasa timu inafika mbele haraka na kutengeneza nafasi nyingi, so kocha apewe muda.
Nakifunga kitabu changu cha takwimu kwa kuhusanisha na mitazamo ya mashabiki, na kuamini kuwa Man United leo itapata ushindi japokua unaweza usizidi bao 3, kutokana na mpinzani wanaecheza nae ambae katika mechi 8 zilizopita ameonekana kuwa mgumu wavu wake kuguswa.
Let’s wait and see, Pira Amorim litatupa majibu gani
Shaffih Dauda