✍🏻Darajani na Old Trafford jumla yamepatikana magoli 7 : Chelsea 3-0 Aston Villa , Man United 4-0 Everton .
✍🏻Nico Jackson anaendelea kuweka kambani , magoli 8 mpaka sasa kwenye EPL
✍🏻Enzo Fernandez performance zake zinaendelea kuwa bora baada ya kufunga leo , katika mechi zake 4 zilizopita amefunga magoli mawili na assists 5 ( amechangia magoli 7 ) . Maresca amemsogeza juu hasa pale Chelsea wakiwa na mpira na kufanya runs zaidi karibu na ndani ya penalty Box
✍🏻Chelsea wamepanda mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa EPL , alama 25 , sita pungufu ya kinara Liverpool ambaye amecheza mechi moja pungufu
✍🏻Unakumbuka mara ya mwisho Man United kufunga magoli 4 kwenye mchezo mmoja wa EPL ? Kila la heri . Chini ya Ruben Amorim wametoa adhabu kwa Everton 4-0
✍🏻Magoli mawili kutoka kwa washambuliaji wao : Rashford mawili na Zirkzee mawili . Na assists mbili kutoka kwa Amad Diallo ambaye leo alikuwa katika kiwango bora sana kutokea nafasi / Jukumu la Wingback .!
✍🏻Cleansheet ya sita kwa Andre Onana katika EPL msimu huu mpaka sasa .!
✍🏻Nafikiri bado ni nyumba ambayo inajengwa ndani ya Man United , unaonekana muundo nini wanajaribu kufanya bado haijawa sawa sawa ( Everton walikuwa wanakatiza mara kadhaa tena kwa urahisi sana , inahitajika maboresho sana lakini Amorim anahitaji muda )