Matukio Haya Kadhaa Yanaonesha Huenda Harmonize na Malaika Wanapika na Kupakua

Matukio Haya Kadhaa Yanaonesha Huenda Harmonize na Malaika Wanapika na Kupakua


Mahusiano ya Harmonize na mrembo Malaika yamekuwa yakivutia hisia na mijadala mingi tangu ukaribu wao ulipoanza kuonekana hadharani. Ingawa bado hakuna uthibitisho rasmi, matukio kadhaa yanazidi kuashiria uwezekano wa mahusiano ya kimapenzi kati yao. Hii hapa ni timeline ya matukio muhimu:


1. Ukaribu wa Kwanza Kupitia Instagram

Harmonize alianza kuhusishwa na Malaika baada ya kushea video ya Malaika akiwa studio anapigwa picha na wimbo unaosikika ni 'You Better Go' wa Harmonize, Ujumbe uliotolewa kwenye posti hiyo ya Oktoba 14, ulionekana kuwa wa mahaba zaidi ya kazi, na mashabiki walichukulia kama hatua ya kwanza ya uhusiano wao.


2. Tukio la Malaika Kupokea Tuzo

Kwenye shherehe ya tuzo za muziki Tanzania, Malaika alifanya hatua isiyo ya kawaida kwa kupokea tuzo ya Harmonize kwa niaba yake. Tukio hilo lilizua gumzo, wengi wakiona hatua hiyo kama ishara ya wazi ya nafasi maalum ya Malaika kwenye maisha ya Harmonize.


3. Video ya Kimahaba - Wimbo 'Wangu'

Video zinazosambaa kupitia insta story ya Harmonize zinawaonyesha Harmonize na Malaika wakifurahia muda wa karibu kimahaba. Video hiyo ilikuwa imeambatana na wimbo 'Wangu' kutoka kwenye albamu ya 'The Godson' ya Marioo, jambo lililoonekana kama njia ya Harmonize kueleza hisia zake kwa mashabiki bila maneno ya moja kwa moja.


4. Malaika - Mpenzi Mpya wa Harmonize?

Kufuatia mfululizo wa matukio haya, mashabiki wengi wanaamini kuwa Malaika ni chaguo jipya la mapenzi kwa Harmonize. Urembo wake na umbo lake vinadhihirisha aina ya mwanamke anayevutiwa naye. Huku wakizidi kuonekana pamoja, bado mashabiki wanasubiri tamko rasmi kutoka kwao.


Kwa sasa, Harmonize na Malaika wanaonekana kuwa na uhusiano wa karibu zaidi ya kazi, huku kila tukio likizidi kuibua maswali zaidi kuhusu mustakabali wa ukaribu wao. Je, ni mapenzi au kazi tu? Muda utaeleza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad