Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTz Taifa Freeman Mbowe @freemanmbowetz amesema anatarajia kukutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari waandamizi Jumamosi ya Desemba 21.2024 kwa ajili ya kutoa msimamo wake endapo atatetea au hatatetea nafasi yake katika mchakato wa ndani wa uchaguzi wa chama hicho unaoendelea
Mbowe ameeleza hayo leo, Jumatano Desemba 18.2024 akiwa nyumbani kwake Mikocheni, jijini Dar es Salaam wakati ambao Wenyeviti wa CHADEMA kutoka kwenye mikoa 21 nchini wamefika nyumbani hao wakiwa na viongozi wengine wa chama hicho wa ngazi mbalimbali kwa ajili ya kumshawishi kutetea kiti hicho
Mbowe amesema, kwa muda mrefu amekuwa akitafakari kuhusu suala hilo hasa baada ya kuona kile kinachoendelea kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ambapo kwa namna moja au nyingine amekuwa akishuhudia 'matusi' na lawama lukuki dhidi yake jambo ambalo linashangaza
Mbowe ametoa rai kwa wafuasi wa chama hicho hususani wale wanaomuunga mkono yeye kuwasamehe wale wote wanaotoka matusi na lugha zisizofaa dhidi ya Mbowe na kwamba mara zote wanapaswa kutambua kuwa wote ni wanachama wa CHADEMA na wana jukumu la msingi la kuhakikisha chama hicho kinaendelea kuimarika zaidi
Hata hivyo, Mbowe amesema licha ya kwamba atatoa msimamo wake wa jambo hilo Jumamosi lakini pia amesema endapo atashuhudia chama chake kinaenda mrama haraka iwezekanavyo atachukua fomu ya kugombea