"Niseme ukweli mara kadhaa nimekuwa na wakati mgumu na familia yangu mwenyewe, hakuna kipindi familia yangu imenishikilia mguu upande kama kipindi hiki (cha mchakato wa uchaguzi wa ndani wa CHADEMA)" -Mbowe
"Wananiambia baba inatosha sasa, inatosha achana na siasa, rudi nyumbani uendelee na maisha mengine, sasa familia yangu nayo ina nguvu katika maisha yangu lakini vilevile familia ya CHADEMA ina nguvu sana katika maisha yangu, zote ni familia zangu na nimeishinazo kwa siku zote" -Mbowe
Mwenyekiti wa CHADEMA @ChademaTz Taifa Freeman Mbowe @freemanmbowetz akizungumza na Wenyeviti wa mikoa 21 wa CHADEMA waliofika nyumbani kwake kumshawishi kutetea kiti hicho leo, Jumatano Desemba 18.2024