Mbwana Harusi Aliyejipoteza Akutwa Kwa Mganga wa Kienyeji Kigamboni

Mbwana Harusi Aliyejipoteza Akutwa Kwa Mganga wa Kienyeji Kigamboni

Mbwana Harusi Aliyejipoteza Akutwa Kwa Mganga wa Kienyeji Kigamboni

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema December 15,2024,lilimpata na kumshiklia Vicent Peter Massawe maarufu Baba Harusi Mkazi wa Kigamboni kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na wizi wa kuaminiwa baada ya kutengeneza mazingira ya uongo ya kupotea na kutengeneza hisia

kwa umma kuwa ametekwa na baadaye kwenda kujificha Pemba Chakechake Mgogoni kwa Mganga wa kienyeji aitwaye Hamis Khalid.


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne amesema “Ufutiliaji na mahojiano ya kina kati ya Polisi na Mtuhumiwa baada ya kupatikana alikiri kutenda makosa hayo ambapo alichukua pesa kwa udanganyifu kutoka kwa Watu mbalimbali ikiwa ni pamoja Tsh mil.55 na gari namba T 642 EGU aina Toyota Ractis kwa udanganyifu kutoka kwa Sylivester Massawe, Tsh. mil. 10 kwa udanganyifu kutoka kwa Ramadhani Mkazi wa Magomeni, Tsh. mil.15 kutoka kwa Ramadhani Bakari Mkazi wa Temeke”


“Mtuhumiwa alichukua pesa pia kwa udanganyifu mil.5 kutoka kwa Resma

Mbuguni HR CBE, mil.4 kutoka kwa Asia Mohamed Mkazi wa Madale, mil.1.5 kutoka kwa Ngoma Mkazi wa Kibaha, pia aliendelea tena kwa udanganyifu kuchukua mil.8 kutoka kwa Fauz Suleimani Mussa Mkazi wa Tabata baada ya kumuuzia gari ambalo sio lake aliloliazima siku ya harusi yake, gari namba T642 EGU Ractis mali ya Sylivester Massawe”


“Ikumbukwe kuwa November 19, 2024 Polisi Kigamboni ilipokea taarifa ya kupotea kwa Vicent Peter Massawe Mfanyabiashara ambaye ilidaiwa hakuonekana toka November 18, 2024 baada ya harusi yake na alipotea huku akitumia gari Toyota Ractis no T 642 EGU ya Sylvester Masawe ambayo baadaye ilibainika aliiuza badala ya kuirudisha kwa mwenyewe baada ya harusi yake November 16, 2024, uchunguzi wa mashauri haya unaendelea na Mtuhumiwa atafikishwa katika Mamlaka nyingine za kisheria kwa hatua zaidi”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad