MKE wa Daisle Simon Ulomi Aliyepotea Tanga December 11 Afunguka

MKE wa Daisle Simon Ulomi Aliyepotea Tanga December 11 Afunguka

MKE wa Daisle Simon Ulomi Aliyepotea Tanga December 11 Afunguka

Munisi ambaye ni Mke wa Mfanyabiashara aliyepotea tangu December 11,2024 Jijini Dar es salaaam, Daisle Simon Ulomi, ameiomba Serikali kupitia Vyombo vya Ulinzi na Usalama kuendelea na uchunguzi huku pia akiwasihi Wadau wa Haki za Binadamu na Watanzania wote kuendelea kupaza sauti ili Mumewe apatikane akiwa mzima.


Akiongea leo December 15,2024 Jijini Dar es salaam kwenye mahojiano maalum na Mwandishi wa @AyoTV_ Bakari Chijumba, Mke wa Ulomi amesema “Tulitoka wote nyumbani tukaenda kwenye eneo letu la biashara Sinza Kijiweni, saa 6:00 mchana tukapigiwa simu na Wakala anayetusaidia kutoa mzigo wetu wa vifaa vya ujenzi kwa ajili ya nyumba yetu ambao umetoka China, Wakala akatuambia TRA wamefungua kontena wameona kuna vitu kama vioo kwahiyo wakati wanakagua watashusha baadhi ya vitu kwahiyo ili kujitoa kwenye shida wanaomba mwenye mali awepo”


“Mume wangu akaondoka kuelekea Mbagala, Bandari kavu kwenda kukagua kontena hilo akitumia pikipiki namba MC 415 DQC aliyokuwa akiendesha mwenyewe, kufika saa tisa alasiri Wakala akanipigia kwamba hadi sasa hivi huyu Mumeo hajafika nikamwambia ameondoka saa mbili zilizopita alitakiwa awe amefika, nami nikapiga hakupatikana, hadi saa 12 jioni Wakala ananiambia naona leo imeshindikana nafunga hili kontena, tukaanza kuuliza kwa Rafiki zake hatukufanikiwa, tukazunguka vituo vya Polisi na Hospitali mbalimbali kwenye vyumba vya kuhifadhi maiti kwamba labda amepata ajali kote hatukumuona”


“Mume wangu hayupo kwenye mitandao sio Mtu wa mitandao kwamba ameandika kitu kimkakera Mtu, sio Mwanachama wa Chama chochote ni Mtu wa kawaida kabisa hana kitu chochote, kabla ya tukio hajawahi kutishiwa na Mtu wala kuniambia kuwa ana ugomvi na Mtu, hanywi pombe na sio Mtu wa Marafiki kabisa nashangaa sana hiki kitu kimekaaje, ni Baba wa Watoto wanne kwahiyo tunateseka hata Watoto sijawaambia wanajua Baba amesafiri, naomba mtusaidie kumpata, Mh. Rais Mama Samia atusaidie najua mkono wa Serikali ni mrefu watusaidie kumpata, kila kitu kimesimama, atakeyemuona anipigie namba 0743996650”


Tayari Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi wa kumpata Ulomi na limeomba mwenye taarifa kuhusu Ulomi azitoe kwenye Mamlaka za Serikali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad