Tabora united leo, Desemba 13 imeweza kupata ushindi finyu baada ya mchezo wao wa leo dhidi ya Azam FC. Kulingana na taarifa tulizozipata hivi sasa, Tabora united imepokea ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Azam FC.
Azam FC wapo kwenye nafasi ya kwanza ikiwa na alama 30. Azam FC wameshinda michezo tisa, wamepoteza mechi mbili huku wakisare mitatu. Simba SC pia wapo kwenye nafasi ya pili wakiwa wamepoteza mechi tisa, wameenda sare mechi moja na kupoteza mchezo mmoja. Hadi sasa wapo alama ishirini na nane.
Klabu ya Yanga pia ipo kwenye nafasi ya tatu huku wakiwa wamecheza mechi kumi na moja, wameshinda michezo tisa na wamepoteza mechi moja.
Tanzania Prisons wapo kwenye nafasi ya kumi na tatu, Kagera Sugar, Namungo FC, KenGold FC wapo kwenye nafasi ya 14,15 na 16 mtawalia.