Muathirika wa P Diddy Aamua Kujiweka Wazi

Muathirika wa P Diddy Aamua Kujiweka Wazi


Anna Kane, mke wa zamani wa staa wa NHL Evander Kane, ameamua kuweka wazi jina lake kwenye mashtaka aliyowasilisha dhidi ya Sean "Diddy" Combs, Harve Pierre, na mtu mwingine asiyetajwa. Mwanzo, alitumia jina la bandia “Ms. Doe” alipowasilisha malalamiko hayo Desemba 2023.

Anna, ambaye sasa ameweka wazi mashtaka yake, anadai kuwa alinyanyasika kijinsia na Diddy na wenzake alipokuwa na umri wa miaka 17, mwaka 2003. Kwenye kesi hiyo, anasema alipelekwa kwenye studio ya Daddy’s House Recording Studio huko New York, alikodaiwa kuleweshwa kwa dawa na pombe kabla ya kunyanyaswa kimwili.

“Nilitarajia kutumia jina la bandia kufanikisha haki juu ya yaliyotokea nikiwa kijana mdogo,” alisema kupitia wakili wake. “Hata hivyo, jaribio la kunilazimisha kutumia jina langu lilikuwa ni njia ya kunitisha. Sitishiki.”

Sean "Diddy" Combs, ambaye kwa sasa anakabiliwa na mashtaka mengine ya ulanguzi wa binadamu na uendeshaji wa ukahaba, amekana madai hayo, akisema kuwa ni juhudi za "kuharibu jina lake na sifa yake."

Mashtaka haya yameibua mjadala mkubwa, huku Anna Kane akitaka wahusika kuwajibishwa kwa kile anachoeleza kuwa ni tukio la kumuumiza kwa zaidi ya miaka 20.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad