Mwanamke Aliyetapeli Mabachela India na Kujipatia Fedha Akamatwa

Mwanamke Aliyetapeli Mabachela India na Kujipatia Fedha Akamatwa


Mwanamke mmoja kutoka India, aliyetajwa kwa jina moja la Seema amekamatwa na Polisi baada ya kugundulika kuwa alitumia ndoa kama njia ya kutapeli Mabachela matajiri kwa kukubali kuolewa na Wanaume waliokuwa wakitafuta Wake akikusudia kujipatia mali kwa kutumia ndoa ili kuwalaghai.


Inadaiwa kuwa Seema alianza utapeli huo mwaka 2013 alipokubali kufunga ndoa na Mfanyabiashara mmoja lakini baadaye alifungua kesi na kudai fidia ya rupia laki 7 (takribani shilingi milioni 21 za Kitanzania) baada ya kutengana na Familia ya Mfanyabiashara huyo kisha aliendelea kutapeli kwa kufunga ndoa na Mhandisi wa Programu kutoka Kampuni ya Gurugram ya India mwaka 2017 ambapo pia baadaye alifungua kesi baada ya kuachana naye kwa kusudi na kudai fidia ya rupia laki 1 (shilingi milioni 2.8).


Mnamo mwaka 2023 alifunga ndoa na Mfanyabiashara mwingine kutoka Jaipur na kisha kutoroka na vitu vya thamani pamoja na fedha akisababisha hasara yenye thamani ya rupia laki 3 (shilingi milioni 10 za kitanzania) ambapo Familia ya Mfanyabiashara huyo iliripoti tukio hilo kwa Polisi na baada ya uchunguzi, Seema alikamatwa.


Katika uchunguzi wa Polisi imebainika kuwa Seema alitumia majina tofauti ili kuwadanganya Wanaume hao waliotalikiwa au waliopoteza Wake zao ambapo katika kipindi cha miaka kumi Mwanamke huyo alikusanya jumla ya rupia milioni 1.25 (takribani shilingi milioni 35 za Kitanzania) kupitia ndoa za ulaghai.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad