Katika operesheni kubwa ya uokoaji, manusura 29 wakiwemo watoto wawili waliokolewa kutoka kwenye mabaki ya ndege hiyo, Naibu Waziri Mkuu wa Kazakhstan, Kanat Bozumbayev, alisema, na kuongeza kuwa 11 wako katika hali mbaya.
Ndege ya Azerbaijan Airlines, safari ya J2-8243, ilikuwa ikisafiri kutoka mji mkuu wa Azerbaijan, Baku, kuelekea Grozny katika eneo la Chechnya nchini Urusi kabla ya kutua kwa dharura umbali wa takribani kilomita 3 (maili 1.8) kutoka Aktau, shirika hilo la ndege lilisema.
Picha za eneo la ajali zilionyesha wakati manusura waliokuwa wameduwaa walipojitokeza kutoka kwenye mabaki ya ndege iliyoteketea.
Manusura wote wamepelekwa hospitalini, mamlaka za Kazakhstan zilisema mapema. Hakuna kati ya manusura walio raia wa Kazakhstan, alisema Naibu Waziri Mkuu.
“Miili iko katika hali mbaya, imeungua sana, yote imekusanywa,” Bozumbayev alisema. “Sasa itakuwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti, na utambuzi utafanyika.”