Polisi Watoa Ufafanuzi Video Inayosambaa Polisi Wakimfukuza Mwanasheria Lusako Alphonce

Polisi Watoa Ufafanuzi Video Inayosambaa Polisi Wakimfukuza Mwanasheria Lusako Alphonce


Jeshi la Polisi limetolea ufafanuzi video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii pamoja na kauli ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Reach Out Tanzania, Kumbusho Dawson ambaye alisema Watu waliojitambulisha kuwa ni Askari Polisi walivamia Ofisi za Taasisi hiyo zilizopo eneo la Makumbusho Jijini Dar es salaam leo wakimtafuta Mwanasheria wa Taasisi hiyo aitwae Lusako Alphonce.


Taarifa ya Polisi imesema ni kweli Askari Polisi walifika eneo hilo kumkamata Mtuhumiwa anayejulikana kwa jina la Emmanuel Mweta ambaye awali alikamatwa na baada ya kudhaminiwa aliruka dhamana kwa muda mrefu.


“Mlalamikaji alitoa taarifa Polisi kuwa amemuona Mtuhumiwa huyo, ikabidi Askari wawahi haraka kumkamata, tunaendelea na uchunguzi kubaini ni nini kilichomfanya anayetajwa kwa jina la Alphonce Lusako kukimbia kisha kujirekodi video voice na kuirusha kwenye mitandao wakati siyo yeye aliyekuwa anatafutwa na Askari waliofika pale walijitambulisha kwake na kumweleza wamefika pale kwa nia ya kumtafuta Emmanuel Mweta” - imeeleza taarifa ya Polisi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad