Polisi Yakamata Wanne Mauaji ya Afisa TRA Tegeta



Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawashikilia Watuhumiwa wanne akiwemo Deogratius Paul Masawe (49), Mkazi wa Tegeta kwa ndevu na Idd Bakari (30), Mkazi Tegeta kwa ndevu ambao wote ni Makuli, pia Omar Issa (47) Mpiga debe Mkazi wa Tegeta Dawasco na Rashid Mtonga (29) Dereva bodaboda Mkazi wa Bunju kwa tuhuma za kufanya mauaji ya Mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aitwaye Amani Kamguna Simbayao pia kumjeruhi Adriano Fredrick wa TRA.

Taarifa iliyotolewa leo December 07,2024 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne Muliro imeeleza yafuatayo “Watuhumiwa hao na wengine ambao bado wanahojiwa kwa kina walikamatwa baada ya kuwashambulia Maafisa hao wa TRA wakati wakitekeleza majukumu yao ya kisheria, waliliharibu pia gari STL 9923 Toyota Land Cruiser mali ya Mamlaka ya Mapato Tanzania”

“Tukio hilo lilitokea Decemner 05, 2024 majira ya saa 03 :00 usiku Tegeta kwa Ndevu Kinondoni baada ya Maafisa hao wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kukamata gari T 529 DHZ aina ya BMW rangi nyeupe lililodaiwa kuwa na makosa ya kikodi, Jeshi la Polisi Kanda maaalum ya Dar es Salaam linawaonya vikali na halitavumilia Watu ambao wanataka kujenga tabia ya kuwashambulia Watumishi wa Serikali wakati wakitekeleza majukumu yao licha ya kuwa wanakuwa wamefuata taratibu zote za kisheria, Jeshi halitasita kuchukua hatua kali za haraka na za kisheria dhidi ya Wahusika kwa kuwafikisha kwenye Mamlaka nyingine za haki” ——— Kamanda Muliro.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad