Rais Samia Suluhu Hassan amemshauri Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi, kujiandaa kuchukua nafasi ya kimataifa iliyoachwa wazi na Dk. Faustine Ndugulile, aliyekuwa Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, kabla ya kufariki dunia Novemba 27,2024.