Rais Samia Amtangaza Profesa Janabi Kugombea nafasi ya Ndugulile WHO – Video

 

Rais Samia Amtangaza Profesa Janabi Kugombea nafasi ya Ndugulile WHO – Video

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kwamba Profesa Mohamed Janabi atakuwa mgombea wa nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika katika uchaguzi utakaotangazwa na shirika hilo.

Rais Samia amesema hayo leo Desemba 10, 2024 baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali wateule wakiwemo mawaziri na manaibu wao.

Profesa Janabi ambaye ni Mshauri wa Rais masuala ya Afya na Tiba na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, atagombea nafasi hiyo kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mteule, Dkt. Fastine Ndugulile aliyefariki usiku wa kuamkia Novemba 27, 2024.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad