Katika kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru leo Desemba 9, 2024 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametumia Mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(a) - (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa msamaha kwa wafungwa elfu moja mia tano na arobaini na nane (1548) ambapo Wafungwa ishirini na mbili (22) kati yao wanaachiliwa huru leo tarehe 9 Disemba, 2024 na elfu moja mia tano ishirini na sita (1526) wanabaki gerezani kumalizia sehemu ya kifungo kilichobaki baada ya kupewa msamaha huu.
"Ni matarajio ya Serikali kuwa wafungwa hao watarejea tena katika jamii kushirikiana na wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa letu na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani" - Imeeleza taarifa iliyotolewa na Wizara ya mambo ya ndani ya Nchi.