ROONEY UKOCHA SIO FUNGU LAKE
Rasmi aliingia kwenye ukocha msimu wa 2020-2021
Timu pekee aliyofundisha kwa misimu mingi ni Derby country [ Misimu miwili ] 2020-2022. Alifukuzwa.
Akahamia DC UNITED alidumu msimu mmoja - 2022/2023. Alifukuzwa fastaaaaaa..
Akahamia BIRMINGHAM CITY msimu mmoja - 2023/2024. Alitimuliwa kama mwizi..
Rooney hakukoma, aliona yeye bado ukocha unaweza kumpa hela baada ya kustaafu soka
May 25 mwaka huu alisaini kuwa kocha mpya wa Plymouth Fc timu ya Ligi daraja la kwanza Uingereza
Tangu awe kocha mkuu wa timu hii, Rooney amekua kocha ambae ni mtaalamu wa kupokea vichapo.
Mechi 10 zilizopita, kashinda mechi 2 pekee.
Huku akipokea vichapo vizito;
Vs Norwich alikufa 6-1
Vs Bristol City alikufa 4-0
Kwenye hizo Mechi 2 karuhusu bao 10
Timu inashika nafasi ya 21 kwenye ligi na wala haina dalili ya kufanya vizuri.
Plymouth wanafikiria kumfukuza, japokua wamempa mechi 2 za kujitafakari
ROONEY FUNGU LA KUKOSA, AHAMIE KWENYE BOXING.