Sakata la Gari la TRA na Watumishi Wake Kushambuliwa Wakidhaniwa ni Watekaji, TRA Wafunguka
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema gari yake yenye namba za usajili STL 9923, ikiwa na Watumishi watatu katika doria za kawaida za udhibiti na ukamataji wa magendo na magari yaliyoingia nchini kinyume na taratibu za forodha na kutolipiwa ushuru, imeshambuliwa na Watumishi kuumizwa katika eneo la Tegeta kwa Ndevu, Dar es salaam December 05, 2024 usiku.
Taarifa iliyotolewa usiku huu na TRA imenukuliwa kama ifuatavyo “Kadhia hii imetokea baada ya Watumishi wa TRA kubaini kwamba gari namba
T229 DHZ aina ya BMW X6 lililoingizwa nchini kinyemela bila kulipa kodi za Serikali stahiki kwa mujibu wa sheria na kuifuatilia kwa lengo la kuikamata ili kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za kodi”
“Wakati Watumishi wa TRA wanatimiza wajibu wao, walihusishwa na kitendo cha utekaji, kilichopelekea wao na gari kushambuliwa, Mamlaka ya Mapato Tanzania inawapa pole Watumishi wake waliojeruhiwa wakiwa wanatimiza wajibu wao na wengine wote waliojeruhiwa katika kadhia hii na kuwaombea wapone kwa haraka, Mamlaka ya Mapato Tanzania inauhakikishia umma kuendelea kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria