Shaffih Dauda: FADLU Ananipa Mashaka, Japo Wameshinda ila Ubora wa Timu Upo Chini Sana


Shaffih Dauda: FADLU Ananipa Mashaka, Japo Wameshinda ila Ubora wa Timu Upo Chini Sana

Mechi ya pili mfulululizo Simba ikiwa nyumbani kombe la shirikisho. Mechi inaisha, Simba ameshinda ila mashabiki wa Simba wameweka mikono kichwani. Badala ya kufurahia wanasikitika.

Mashabiki hawajaridhika, kiwango cha uchezaji kipo chini mno. Kiufundi tatizo la Simba linaanzia hapa;

◽️Eneo la midfield kuelekea eneo la mwisho la ushambuliaji. [Progressive Phase]

Mido za Simba muda mwingi zinapiga pasi fupi fupi zisizo na madhara. Hili ni eneo linalohitaji akili, ubunifu, na uharaka wa maamuzi. Simba wapo slow mno, na pia wanakosa watu sahihi kimfumo kufanya hayo.

Jean Ahoua, Ngoma, na Debra leo hawakua na maajabu. Pasi zao nyingi walipiga kuelekea pembeni mwa uwanja [Square passes].

Pembeni Simba ilikua imekufa, kati ilikufa. Achana na magoli mawili ya Kibu. Je alitengeneza nafasi ngapi za magoli yeye kama winga?

Fadlu ilibidi afanye tactical switch za kuwaingiza Kagoma, Nouma, na Karabou ili wapate uhai. Lakini tazama aina ya sub za Simba zinaonyesha kabisa Simba inakosa options kwenye benchi, wachezaji wenye hatari wanaoweza kubadili matokeo, nikimaanisha wachezaji kwenye eneo la ushambuliaji.

Huwezi kumlaumu Ateba au Mukwala. Jiulize Simba inatengeneza nafasi ngapi kwa strikers wao? Je nafasi wanazotengeneza Simba zina ubora wa kutosha kumrahisishia kazi striker? Jibu ni HAPANA

Ahoua, Awesu wametengeneza nafasi ngapi kwa Mukwala? Wao kama viungo wabunifu hawakua na hatari yoyote. Kwangu naona Simba inahitaji kusajili number 10 anaeijua kazi yake vizuri. Ahoua ana namba nzuri [ Goals & Assists] ila bado level yake ipo chini sana quality wise.

Mashaka anayonipa Fadlu ni kuwa ameshindwa kutengeneza namna nzuri ya Simba kushambulia lakini bado timu haichezi vizuri. Simba inaingia na wachezaji wachache kwenye box la mpinzani. Fadlu bado anahitaji kutuonyesha ubora wake zaidi kwenye mbinu zake, kwa sasa bado anacheza chini ya matarajio.

YES! Simba ana points 6 kwenye group lake, lakini Kwa mwendo huu wa kuchechemea, kuna mahala itafika itakua ngumu Simba kupata matokeo.

MUDA UTAONGEA.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad