Shaffih Dauda "Labda Yeremia 33:3 Ndio Itawasaidia Yanga Leo Mbele ya TP Mazembe"

Shaffih Dauda "Labda Yeremia 33:3 Ndio Itawasaidia Yanga Leo Mbele ya TP Mazembe"


Misukosuko na kukosa tumaini, labda na kukata tamaa kunawezekana kupo mioyoni mwa klabu ya Dar Young Africans

Unapoutazama msimamo wa kundi lao kwenye mashindano ya CAF inasikitisha kidogo. Mechi 2, wamefungwa 2, na kuruhusu bao 4, huku wakiwa hawajafunga bao lolote.

Unapotazama kuwa kati mechi 5 zilizopita za mashindano yote wamefungwa mechi 4, na kushinda moja pekee vs Namungo, inazidi kutia huzuni kubwa. Kuanguka kwa Yanga, Maswali yanakua mengi kuliko majibu

Sidhani kama itasaidia tukielezea mechi hii kiufundi leo kama Yanga hawatomtanguliza Mungu mbele kwa sala na maombi makali kwanza.

Ningewaomba wafungue maandiko matakatifu mstari wa Yeremia 33:3 ambao nao unasema. ”Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua”.

Neno hili linatuasa kuwa tunapopitia kipindi kigumu ni nyakati sahihi kumrudia Mungu mwenyezi ili atujaalie ufunuo wa kufanikisha na kuvuka vikwazo. Kwa sasa Yanga imekwama, inakosa majawabu ya mambo yao magumu wanayopitia. Ni Sala pekee itakayowavusha.

Yanga ipo katika wakati mgumu sana, kama ikifungwa leo, safari yao kwenye mashindano ya CAF uwezekano ni mkubwa itakua imeishia hapo.

Dube aongoze hii sala

Duke Abuya ataanza na pambio la kusifu na kuabudu.

Aziz Ki afunue Yeremia 33:3

Diara afunue Yeremia 33:3

Aucho afunue Yeremia 33:3

Wanaweza kuwa wanaujua sana mpira, wamefanya sana mazoezi, wameahidiwa bonus kubwa sana, ila kwa hatua iliyofikia Yanga kwa sasa ni MAOMBI tu

Mungu baba wa mbinguni akawaongoze leo hii kupambana kwa kadri ya uwezo wao.

GUSA ACHIA TWENDE KWAO IENDE IKABARIKIWE SIKU YA LEO.

AMEN.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad