Shaffih Dauda, Licha ya Kushinda Ukuta wa Yanga Una Tatizo, Kibwana Kacheza Vizuri


Kibwana
Yanga kushinda wala sio story. Ilikua ni lazima washinde. Yanga ilikua inaingia kucheza na timu ambayo ndani ya mechi 14, imeshinda mechi 4, na sare 3 mfululizo katika mechi zao 3 zilizopita.

Yanga kuruhusu bao mbili kutoka kwa Mashujaa waka sio story, imekua kawaida yao hivi karibuni. Katika mechi 7 zilizopita, Ni mechi 1 tu dhidi ya Namungo ambayo walimaliza na ‘Clean-sheet’. Ila mechi 6 zilizobakia Yanga wameruhusu bao jumla ya bao 11.

Kuhusu kuruhusu bao, Yanga imeanza kufanya hvyo Gamondi akiwa kwenye utawala, na imeendelea kufanya hvyo Ramovic akiwa kocha mpya. Mbaya zaidi, Diara na Khomeiny, wote wameonekana kufikika kirahisi golini.

Hata bao za leo ambazo wameruhusu Yanga huwezi kumtupia lawama kipa Khomeiny. Jaribu kutazama mazingira ya goli kupatikana yalikuaje. Mashujaa wamefikaje kupata nafasi za ku’attempt?

Kimsingi, tatizo la Yanga limekua katika mfumo wa ulinzi.

Kuhusu, Kibwana Shomari. Amecheza vizuri sana na upande wako haukua sehemu ya kusababisha Yanga ishambuliwe. Uwezo wa kusapoti mashambulizi ( Left link up plays) alivyokua anacheza na Mzize, na baadae Pacome ilikua super sana. Je ataendelea kuaminiwa kucheza nafasi hiyo chini ya Ramovic? Je ataendelea kupata nafasi mara kwa mara. Ni suala la kusubiri na kuona

Dube Hat-trick. Mimi binafsi niliamini Dube atakuja kufufuka kutoka kwenye kifo cha kushindwa kutumia nafasi. Imani yangu ilitokana na ukweli kwamba Dube mara zote hakua anacheza hovyo, overall game yake haikua na shaka. Hold-up play, positioning na movements zake mara zote zilikua on point, alichokua anakosa ni kutumbukiza mpira wavuni. Mechi 2, Bao 4 - Mwana Mfalme katoka kwenye maombi ya Nabii Mutalemwa, anafanya kweli. Good day in the office.👍

Ramovic bado ana kazi ya kufanya. Yanga inafikika kirahisi sana pale nyuma. All in all, points 03 muhimu za kuendelea kurudisha morali kikosini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad