Siku 27 za Mateso Makubwa Kwa Man United Zinakuja, Amorim Atawavusha Nchi ya Ahadi?

 

Siku 27 za Mateso Makubwa Kwa Man United Zinakuja, Amorim Atawavusha Nchi ya Ahadi?


Kuanzia tarehe 15 Dec 2024 mpaka 12 Jan 2025 zitakua siku za utakaso na kupima imani kama kweli Amorim ndiye atakaewavusha mashetani wekundu kufika nchi ya ahadi.


Jumla zitakua siku 27 zinazoweza kuwa za furaha au huzuni kuu kutegemea na namna wana wa Amorim watakavyofuata na kuwa na imani na mfumo wake dhidi ya wapinzani atakaokutana nao

Nazitama mbingu, napiga magoti huku nikiwaombea wapenzi wote wa Man United wapate faraja mbele ya ratiba hii ngumu ifuatayo.


Dec 15: Man City vs Man United

Dec 19: Tottenham vs Man United


Mpaka hapa Man U atakua anahitaji siku 3 za maombi mazito ili apite salama. Baada ya hapo;


Dec 22: Man United vs Bournemouth

Dec 26: Man United vs Wolves.

Dec 30: Newcastle vs Man United


Baada ya ratiba hii, Man U ataufungua mwaka mpya katika namna ya kipekee sana. Ni wiki ya kwanza ambayo Man U ataimba na kusifu, kuhitaji ukuu wa Mungu umeuepushe na aibu takatifu. Tazama👇🏾


January 05: Liverpool vs Man United

January 12: Arsenal vs Man United


Kwa ratiba hii ningeomba mashabiki wapate neno la matumaini, kutoka ule mstari kwenye biblia takatifu, WAFILIPI 4:13 …. inayosema; NAYAWEZA YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU.


Malizeni kwa kusema AMEN. 🙏

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad