Timu ya Tabora United ni CAF Material, Kama Wapo Wanaoendelea Kuidharau Tabora Bado Hawajaumwa na Nyuki

 

Timu ya Tabora United ni CAF Material, Kama Wapo Wanaoendelea Kuidharau Tabora Bado Hawajaumwa na Nyuki



TABORA UNITED NI CAF-MATERIAL.

Anafunga bao 2 saaafi kabisa. Anainua mikono yake huku akipiga paa, paa, paa. Yani anawajaza. Hapa namuongelea Heritier Ebeneze Makambo na Tabora United yake wakimpasua Azam Fc na kuwalambisha asali nyuki wadogo kutoka Tabora.


Sasa habari hapa sio migoli ya kiroho mbaya ya Makambo, habari ni ubora wa Tabora United. Hii ni timu ni ‘CAF-MATERIAL’ Nitawaeleza mambo kadhaa ya kiufundi kuipa nguvu hoja yangu.


Timu ambayo ina uwezo wa kushindana kwa level kubwa utaipima kupitia ubora wa mchezaji mmoja mmoja, team fitness, na muunganiko mzima wa idara zote ndani ya uwanja ( Ukabaji, Eneo la midfield, na Ushambuliaji )


Tabora ilivyokua chini ya Coach Francis Kimanzi ilikua haieleweki inataka nini uwanjani. Ujio wa kocha mpya, Anicet Makiadi umeifufua Tabora.


Anicet Makiadi ameifanya Tabora United iwe timu hatari inapokua na mpira [in-possesion] mido zao hazikai kabisa na mpira. Kazi yao ni touch moja, ya pili mpira ufike kwa mhusika kwa ajili ya kufanyiwa uchakataji wa kupeleka mirindimo ya milio ya nyuki kwenye idara ya ushambuliaji.


Pale Juu unamkuta Yacouba, Chikola, na Makambo, hawa wote ukiwapa mpira mguuni wanajua waufanyie nini, ni proven players ambao walishacheza michezo mikubwa na wana experience ya kuamua mchezo muda wowote.


Tabora wakipoteza mpira hapo ndipo utawapenda wanakua kama mabawa ya nyuki anayeenda kwenye mzinga wake kulala. Winga zote zinafungua mabawa kuukimbiza mpira, mido zinasogea kwa juu, full beki nazo zinaongeza namba kuhakikisha mpira unarudi chini ya himaya yao haraka sana. Tabora wanajua kuzuia vizuri, kuziba channel zote, za ndani na nje ambapo mipira inaweza kupita.


Wakati watu wanashangaa inakuaje Tabora amecheza mechi 6, ametoa sare 1, na kushinda mechi 5 huku vigogo kama Yanga na Azam wakipoteana vibaya mno, mimi sishangai kabisa. Hii Tabora ni ‘CAF-MATERIAL’ imeiva, ikaivishwa halafu ikaiva tena.


Tarehe 17 Dec, Tabora United vs Coastal Union, nategemea bila shaka tabora atapata matokeo wala sitoshangaa.


Kama wapo wanaoendelea kuidharau Tabora wakihisi inabahatisha basi kazi yangu ni kuweka onyo tu kwamba NYUKI HAKUMBATIWI, na MZIGO MZITO MPE MNYAMWEZI.

Shaffih Dauda

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad