TMA Yatoa Utabiri Mpya wa Hali ya Hewa, Mvua Kubwa Mikoa Mitano



TMA imetoa taarifa kuhusu utabiri wa hali ya hewa nchini Tanzania kwa kwa saa ishirini na nne zijazo. Kulingana na taarifa tulizozipata hivi sasa, Kanda ya ziwa Victoria mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara. Maeneo yaliyotajwa yanatarajiwa kupokea vipindi vya mvua zitakazoambatana na ngurumo za radi kwanzia leo jioni.

Maeneo ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro yanatarajiwa kupokea vipindi vya mvua nyingi. Pwani ya Kaskazini mikoa ya Tanga, maeneo ya Kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba; vipindi vya mvua vinatarajiwa katika maeneo machache. Kwa hivyo, TMA imewahimiza wakazi wa maeneo hayo wajiandae ipasavyo.

Mikoa ya Rukwa, Iringa, Njombe, Mbeya na Songwe inatarajia kuwa na hali ya mawingu, mvua na ngurumo za radi katika maeneo machache na vipindi vifupi.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad