Mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi
Baada ya taarifa za kupotea kwa Mfanyabiashara Daisle Simon Ulomi ambaye hakurudi nyumbani kwake toka alipoingia kazini December 11, 2024 Jijini Dar es salaam, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema haihusiki na swala la kupotea kwa Mfanyabiashara huyo.
Taarifa hii ya TRA inakuja baada ya Meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob kuandika kuwa Ulomi amesema aliondoka Sinza kwenda Mbagala Bandari kavu kukagua kontena lake baada ya kuitwa na Watu wa TRA kwa ajili ya ukaguzi.