Tundu Lissu Atoa Taarifa Muhimu Kuhusu Kuhama Chama cha Chadema



Tundu Lissu Atoa Taarifa Muhimu Kuhusu Kuhama Chama cha Chadema
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (Kulia), na makamu wake Tundu Lissu. [Picha: Boniface Jacob/X]

Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, ametangaza kuwa hana mpango wa kuhama chamani, kama inavyodaiwa na wengine.

Kumekuwa na madai kuwa Lissu ana mpango wa kuhama chama, wakosoaji wakidai kuwa hii ndiyo sababu yake kutangaza azma ya uenyekiti.

Wanaoeneza madai haya wanaoongozwa na aliyekuwa Kada wa Chadema, mhubiri Peter Msigwa, ambaye alihama na kujiunga na CCM.

Hata hivyo, Lissu amesema kuwa hana mpango wa kuitoroka chama, akiyapuuzilia mbali madai ya Msigwa kama yasiyo na ukweli wowote.

"Kwanza niweke wazi maana kuna vimaneno maneno kwamba huyu anatengeneza namna ya kuhama, sasa nataka niseme haami mtu hapa. Ukisema Msigwa alisema hivyo hivyo nataka niwaambie Msigwa sio Tundu Lissu," alisema Jumanne.


Mwanasiasa huyo ametoa kauli hiyo alipofanya mahojiano maalum na Clouds FM kupitia kipindi cha Power Breakfast.

Pia ametetea hatua yake ya kuendelea na siasa licha ya changamoto mingi aliyoipitia, akisema kuwa azma yake ni kuboresha Tanzania.

"Mliniuliza baada ya yote hayo, marisasi yote hayo, majela yote haya kwa nini bado umo kwenye mapambano ya siasa na demokrasia."

"Nataka muelewe kwamba nipo kwa sababu nilizaliwa kwa sababu ya kazi hii. Mimi ni mwanamageuzi, na Chama cha Mapinduzi (CCM) hakijawahi kuwa chama cha mageuzi na hakitakaa kiwe cha mageuzi," amesema.

Wakosoaji wake wamedai kuwa azma yake ya uenyekiti inadhamiria kusababisha mgongano na upande wa Mwenyekiti wa sasa Freeman Mbowe, na kumpa Lissu sababu ya kuitelekeza Chadema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad