Ukraine imeonesha kombora lake jipya lililotengenezwa ndani ya nchi linalojulikana kama kombora la droni au ndege isiyo na rubani inayoweza kuruka umbali wa kilomita 700 (maili 430), umbali mrefu zaidi ikilinganishwa na makombora yaliyotolewa na washirika wa Magharibi.
Ndege hiyo isiyo na rubani, inayoitwa ‘Peklo’ ambayo maana yake ni ‘jehanamu’ kwa Kiukreni, ni kombora la pili kuoneshwa na Ukraine wakati ikijaribu kuongeza uwezo wake wa kuishambulia Urusi.