Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema kuna hitilafu katika mfumo wa Gridi ya Taifa leo December 04, 2024 iliyotokea saa 04:03 asubuhi ambayo imepelekea Mikoa inayopata umeme kupitia Gridi ya Taifa kukosa umeme.
Taarifa iliyotolewa na TANESCO leo imesema Wataalamu wake wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha hitilafu hiyo ambapo umeme umeanza kurejea kwa awamu katika Mikoa iliyokuwa inakosa umeme huku jitihada zikiendelea kuhakikisha Mikoa yote inapata umeme mapema iwezekanavyo.
“Shirika linawaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na litaendelea kutoa taarifa za hali ya urejeshaji wa huduma ya umeme kwa kadri hali inavyoimarika” - TANESCO.