Ushauri wa MBOWE Kwa Tundu Lissu....




“Suala la pesa za Mama Abdul na Abdul imezungumzwa sana na haya mambo tumesema hata kwenye vikao vyetu kwamba mwenye ushahidi alete, kuna swali kwamba Makamu Mwenyekiti anasema kuna udhaifu wa Sekretarieti kwahiyo hajaweza kuitisha vikao vya maadili mpaka apelekewe shutuma”

“Makamu Mwenyekiti wa Chama ni Msaidizi wa Mwenyekiti, Watu wawili wanaoweza kumuagiza kazi Katibu Mkuu ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti, kama Makamu ana tuhuma za fedha za Mama Abdul haitaji kumsubiri Katibu Mkuu amletee mashtaka anapaswa amuagize Katibu Mkuu na Sekretarieti yake amuandalie kikao”

“Namshauri Makamu wangu mpaka hapo tarehe 23 anaweza kuwa Boss wangu (akishinda uchaguzi), namshauri ajenge Timu, mchezo wa siasa ni Team Work, unamuhitaji Kipa, Beki na Foward huwezi ukashinda pekee yako bali kwa kusaidana na wenzako, waheshimu wenzako na nafasi zao, tambua mchango wao, usikazane kuwapaka wenzio matope haimpendezi Mungu” — Freeman Mbowe
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad