Mchambuzi Edga Kibwana amepenyezewa taarifa na mdau kuwa kuna baadhi ya wachezaji wa Ligi kuu wamekuwa wakibet mechi zao hali inayopelekea Ligi kuwa na matukio mengi ya kustaajabisha.
Mdau anaziomba mamlaka zinazohusika na Soka kuanza kuchunguza taarifa hizi ili kuwabaini
Kutoka kwa Amri Kiemba:
“Sisi tunaongea huku tunacheka lakini hali ni mbaya , inawezeka tupo hapa tunasema waamuzi waongezewe ujuzi kumbe wao nyuma wanabet”
Katika kuipa uzito hoja yake Kiemba amesema unaweza kushangaa goli ni offside ya wazi lakini mwamuzi anaacha kwa sababu ameweka GG .