Ameandika Wakazi Kupitia Instagram yake:
IT IS NOT FAIR: Ushirikina uko kila mahali kuzidi muziki !!
Sidhani kama ni sahihi kusema Music peke yake ndio una mambo ya KISHIRIKINA hapo Tanzania! Au kwamba kila anayeufanya au aliyefanikiwa amefanya hivyo sababu ya Maagano ya kishetani.
Imani za kimila kweli zipo Tanzania, ila hiyo ni sehemu ya utamaduni wetu. Sidhani kama mambo ya uchawi na kulogana ya kwenye muziki, yanafikia hata robo ya yanayotokea kwenye MAPENZI, SIASA, KAZINI, MICHEZO!!
Watu wanataka kufanikiwa, na wakifikia hiyo desperation ya juu, basi wanaweza kushawishika kufanya lolote ili jambo lao liende. Ila sio wote pia…
Na kingine, sidhani kama kutoa Sadaka au kwenda kwa Sheikh atie Baraka kabla ya kutoa kazi, huo ni ushirikina. Mimi sio Muislamu, ila nina marafiki Wasanii ambao wanafanya hivyo… na naona ni sawa (kuomba kheri kwenye kazi yako).
Ila uchawi upo, maagano ya kishetani yapo, na ni kila mahali kwa wanaoamini na walio desperate enough, au wenye husda juu ya mafanikio ya wengine.
Pia Suala la baadhi nyimbo za dini (“Gospel”) kutosema Yesu, sidhani kama ni sababu ya ushetani. Gospel iligeuka kuwa muziki wa kibiashara na wadau wakubwa walifanya conscious decision ya kuhimiza kusema Mungu ili wasiwatenge baadhi ya walaji, maana tukiwa wakweli, sio Wakristo tu ambao wamekuwa wanafurahia nyimbo za dini. So hakuna conspiracy hapo, maana pia kama hata mahubiri ya kanisani yalivyokuwa sometimes yanahusu maisha, ndoa, mafanikio, nk, hata muziki nao sometimes unatoa mafunzo tu ya kimaisha.
Pengine tukianza ku-appreciate muziki kwa ubora na utofauti wake, badala ya kuwawekea pressure artist kuwa na stereotypical hits, basi wataacha kuwa desperate na kuhamia kwenye uchawi. Ila bottom line sidhani kama ni sahihi kuwanyooshea kidole wao tu… Mambo ya Jadi ni masuala ya nchi.
SWALI: Zamani wahayudi walikuwa wanatoa sadaka kwa kichinja kondoo… ili Mungu awabariki. Je mtu akifanya tambiko la kimila@kwa kuchinja mbuzi kwanini aonekane kafanya kitu cha ajabu?! Je tunatofautishaje good magic & dark magic?! ana pia kuna secular artists wameimba nyimbo ambazo ni sawa na hawa Gospel artists wanazofanya, do we accept their songs as gospel? ( Phina - “Sisi Ni Wale”, MwanaFA - “Mfalme”)