Wamasai Sasa Ruksa Kuoa, Kuolewa na Waswahili

Wamasai Sasa Ruksa Kuoa, Kuolewa na Waswahili


Mjumbe wa serikali ya Kijiji cha Mserekia, Easter Lenana akizungumzia uamuzi huo wa kimila.

SIKU 16 za uanaharakati, kupinga ukatili wa kijinsia mkoani Kilimanjaro, zimepata mjongeo chanya, baada ya wafugaji wa jamii ya Kimasai wanaoishi ukanda wa chini wa Moshi, kuanza kuiweka kando sheria yao ya kimila ya kuwachagulia vijana wa kiume mke, na wasichana kuolewa na mume anayetoa posa tangu akiwa mtoto.


Hivi sasa, viongozi wa mila wa kabila la Wamasai, wameruhusu vijana wao wa kiume, kuoa mke anayempenda kutoka kabila lao au jingine, na msichana kuolewa na mwanamume ampendaye, ambaye hakutoa posa ili kumchumbia tangu akiwa mtoto.


Akizungumza leo katika Kijiji cha Mserekia, Kata ya Mabogini, wakati wa mdahalo wa kutoa elimu ya kupinga ukatili, ambao ni sehemu ya utekelezaji wa siku 16 za kupinga ukatili, mzee wa mila wa jamii hiyo, Legwanani Isaack Daudi, amesema kwa sasa suala la kuolewa na kuchagua mume, ni sawa kijana au msichana wa Kimasai anaweza akachagua.


Mdahalo huo wa kutoa elimu hiyo katika siku 16 za uanaharakati kupinga ukatili, unaendeshwa kupitia Mradi wa Sauti ya Haki, unaotekelezwa na Shirika la KWIECO, kwa ufadhili wa Women Fund Tanzania Trust (WFT).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad