Hoteli hiyo iliyopo katika Mji wa Adiyaman ilianguka mwaka jana wakati wa tetemeko la ardhi.
Aidha mtoto wa mmiliki wa hotel hiyo Mehmet Fatih amehukumiwa kifungo cha miaka 17.
Watatu hao wamehukumiwa kwa makosa ya kusababisha vifo vya watu 72 na majeruhi kwa uzembe walioufahamu.
Wakati hoteli hiyo ikianguka, walikuwemo Watalii pamoja na timu ya mpira wa wavu ya shule, ambapo kati yao walipona walimu wanne tu.