Waziri Mchengerwa Acharuka, Aipinga Vikali Kauli ya Paul Makonda



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, maarufu kama "Mtu Kazi," amejitokeza hadharani na kulaani vikali kauli tata iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.


Mkuu huyo wa mkoa alikuwa amepongeza tukio la kusikitisha ambapo wananchi walimvamia na kumtembeza diwani kwenye matope.

Waziri Mchengerwa amesisitiza kuwa matendo ya aina hiyo si maagizo ya serikali na kwamba viongozi hawapaswi kuhamasisha wananchi kuchukua sheria mikononi.


Akizungumza leo katika mkutano na waandishi wa habari, Mchengerwa alisema, "Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haina sera ya kuchochea vurugu au kutoa adhabu nje ya mfumo wa kisheria.

Kauli kama hizi si tu zinavuruga utawala wa sheria, bali pia zinachochea ghasia zisizo za lazima."

Kauli ya Mkuu wa Mkoa imeibua hasira na masikitiko miongoni mwa wananchi, huku wengi wakishangazwa na uungwaji mkono wa matendo yasiyo ya kistaarabu.

Tukio hilo, ambalo lilisambaa mitandaoni, limeacha doa kwa serikali na kuibua maswali kuhusu uwajibikaji wa viongozi wa ngazi za juu.


Mchengerwa ameongeza kuwa serikali inaendelea kuchukua hatua kuhakikisha viongozi wanazingatia maadili ya uongozi na kusimamia haki kwa kila raia.

Kiongozi yeyote anayevunja miiko ya uongozi atawajibishwa bila kusita.

Hakuna nafasi kwa kauli za kichochezi ndani ya utumishi wa umma," alisisitiza.


Kauli hii ya Waziri inachukuliwa kama onyo kwa viongozi wengine wanaotumia nafasi zao vibaya, huku ikitoa matumaini kwa wananchi kwamba serikali itaendelea kulinda haki na usawa bila kujali daraja la mtu.


Tukio hili linapaswa kuwa somo kwa wote kwamba haki haipaswi kuchezewa.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad