Waziri Mkenda Aingilia Kati Madai ya Wanafunzi Kufukuzwa Shule Kisa Chadema

Waziri Mkenda Aingilia Kati Madai ya Wanafunzi Kufukuzwa Shule Kisa Chadema


Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeeleza kusikitishwa kufuatia taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Izinga, iliyopo kata ya Wampembe, jimbo la Nkasi Kusini, Halmashauri ya wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa wamefukuzwa shule kutokana na kile kinachodaiwa kuwa wazazi wao kuwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)


Mtandao wa Mwananchi digital umechapisha taarifa hiyo leo, Alhamisi Desemba 05.2024 ukieleza mahojiano iliyofanya na Waziri wa Wizara hiyo Prof. Adolf Mkenda ambaye amesema baada ya kuona madai hayo ametuma jopo la wataalamu ili lifike kwenye eneo husika kuchunguza ukweli wa taarifa hizo


"Nimeona taarifa za wanafunzi kwamba wameondolewa shule kwa sababu wazazi wao ni wanachama wa CHADEMA, nimeshangazwa sana na taarifa hii na tayari timu yetu ya wadhibiti ubora (elimu) nimeituma asubuhi hii ifike pale shuleni na ituambie ukweli kuhusu jambo hili" -Prof. Mkenda


Waziri huyo amesema msimamo wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kwamba watoto wote wana haki ya kusoma na kwamba hakuna mtu au kikundi cha watu chenye mamlaka ya kumuondoa mtoto shuleni kwa sababu za kisiasa


Mapema leo Jambo TV imefanya mahojiano kwa njia ya simu na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Nkasi akiwemo Mkuu wa wilaya hiyo Peter Lijualikali ambaye alikana kutambua uwepo wa jambo hilo kwa kuwa kwa wakati huo alikuwa njiani kurejea Nkasi akitokea jijini Dar es Salaam alikokwenda kikazi


Hata hivyo, Mkuu wa wilaya hiyo alimtaka mwandishi wa Jambo TV kuwasiliana na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nkasi kwa kuwa yeye ndiye msimamizi wa watumishi wa umma kwa ngazi ya Halmashauri


Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Izinga Regius Martin Kawimbe anayedaiwa kuandika barua za kuwafukuza wanafunzi hao amesema hakuna mwanafunzi yeyote aliyefukuzwa kwa madai ya kisiasa, isipokuwa alimtaka mwandishi wa Jambo TV kutafuta barua hizo na kuona sababu zilizowekwa ambazo si za kisiasa kama inavyodaiwa


Mwalimu huyo ambaye pia alikuwa Msimamizi msaidizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa ngazi ya kijiji (kijiji cha Izinga) alipoombwa kueleza unda

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad