"Single Pivot ni nzuri sana kuitumia kwa timu dhaifu ambayo haina makali sana kwenye kushambulia wala yenye tabia ya kutumia Counter Attack ku score magoli."
"Nashauri sana Sead Ramovic atumie Double pivot kuliko kutumia single pivot kutokana na aina ya mpinzani anaekutana nae,Mc Alger hupenda sana kutumia Counter Attack kufanikisha kupata mabao."
"Double Pivot huwezesha viungo wakabaji wawili kucheza kwenye line moja na kwa ufanisi wa hali ya juu ambapo hata kama Mc Alger watatumia Counter Attack basi kuanzia kwenye Mid Block kuelekea kwenye Low block kutakua na wachezaji wengi wa Yanga waliosalia ukilinganisha wakitumia Single Pivot."
"Ubaya na uzuri wa kutumia Single Pivot,Single Pivot huwezesha wachezaji wengi kuchezea kuanzia kwenye Mid Block kueleka kwenye High Block jambo ambalo ni rahisi sana kupata mabao lakini ni mbaya sana ikitumika Counter Attack maana wachezaji wengi watakua eneo la juu kabisa (High Block)."
"Ikatokea Counter Attack imekubali basi ni rahisi kiungo mkabaji aliebaki kufanya madhambi yatakayopelekea timu yake kuadhibiwa vibaya au kupitika kirahisi zaidi."
"Nashauri tena kocha Sead Ramovic asitumie Single Pivot atumie Double Pivot,kuhusu mfumo wake wa 4:2:3:1 sina shaka nao kutokana ni mfumo unaowezesha wachezaji kuachiana nafasi (space) na kunyumbulika kucheza pass nyingi na kusoma udhaifu wa mpinzani kirahisi."
Anasema @princendosi17
.